Bow Down | |||||
---|---|---|---|---|---|
Studio album ya Westside Connection | |||||
Imetolewa | Oktoba 22, 1996 | ||||
Imerekodiwa | 1996 | ||||
Aina | Gangsta Rap, G-funk, West Coast Hip Hop | ||||
Urefu | 48:07 | ||||
Lebo | Lench Mob/Priority | ||||
Mtayarishaji | Ice Cube Cedric Samson QDIII Binky Mack Bud'da Mark Jackson Ian Scott |
||||
Wendo wa albamu za Westside Connection | |||||
|
|||||
Single za kutoka katika albamu ya Bow Down | |||||
|
Bow Down, ni jina la kutaja albamu ya kwanza kutoka katika kundi babu-kubwa la West coast hip hop/gangsta rap Westside Connection. Albamu ilitolewa mnamo tar. 22 Oktoba, 1996 kupitia studio ya Ice Cube Lench Mob/Priority Records. Albamu imeshirikisha tayarisho kutoka kwa mtayarishaji kama vile Bud'da, QDIII na Ice Cube na wengine wengi tu.
Albamu ilifika nafasi ya pili katika chati za Billboard 200 mnamo Novemba 9, 1996, nakala zilizoenda nchi za nje ni 145,000.[1] Imeenda kuuza nakala milioni 1.7, na kutunukiwa platinamu na RIAA mnamo Oktoba 1, 1997.[2] Nyimbo kama King of the Hill, Cross 'Em Out na Put a 'K, na Hoo Bangin' (WSCG Style) zote ni nyimbo za kuponda wengine na waliopondwa ni pamoja na Cypress Hill, Q-Tip na Common.